𝑮𝑨𝑽𝑨𝑵𝑨 𝑩𝑨𝑹𝑨𝑺𝑨 𝑨𝑻𝑨𝑲𝑨 𝑺𝑬𝑹𝑰𝑲𝑨𝑳𝑰 𝑲𝑼𝑼 𝑲𝑼𝒁𝑰𝑷𝑨 𝑲𝑨𝑼𝑵𝑻𝑰 𝑴𝑮𝑨𝑶 𝑾𝑨𝑶
Gavana wa jimbo la Kakamega, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha katika Baraza la Magavana nchini, Mstahiki FCPA Fernandes Barasa, ameiomba serikali kuu kuheshimu ugatuzi kwa kutoa mgao wa pesa wa Shilingi Bilioni 81, kiwango ambacho ni wastani wa malipo ya deni la miezi mitatu iliyopita.
Akizungumza katika kanisa la Jeshi la Wokovu, Wadi ya Marama ya Kati, Kaunti ndogo ya Butere, ambapo alihudhuria ibada ya Jumapili na kuongoza hafla ya mchango wa ujenzi wa kanisa hilo, Gavana Barasa ameeleza kuwa kucheleweshwa kwa fedha hizo kumehujumu shughuli mbalimbali katika magatuzi, ambapo Kakamega kuna changamoto katika kutekeleza miradi ya maendeleo na shughuli mbalimbali za uongozi.
Hata hivyo, Serikali ya Barasa imejizatiti na kuhakikisha mishahara ya wafanyikazi wa kaunti inalipwa kwa wakati unaofaa, na pia kuendelea kwa miradi muhimu kama ujenzi wa barabara pamoja na madarasa ya shule za chekechea katika kila wadi, inayo tekelezwa na serikali yake kwa sasa.
Gavana Barasa pia ameonyesha wasiwasi kuhusu ongezeko la majukumu kwa serikali za kaunti, kama vile ukarabati wa vifaa vya matibabu ambao awali ulikuwa unafanywa na serikali kuu; lakini sasa utatekelezwa na serikali za kaunti bila kuongezwa kwa mgao wa fedha.
Barasa alikuwa ameandamana na Wawakilishi wa Wadi wakiongozwa na Mhe. Philip Maina (Mwenyeji na pia Kinara wa waliowengi bungeni), Maafisa wa Kaunti wakiongozwa na Waziri wa Afya Dk. Benard Wesonga, Katibu na Mkuu wa Wafanyikazi wa Umma, Dk. Lawrence Omuhaka
miongoni mwa waumini wengine.