NewsTrending

𝑴𝑨𝑻𝑬𝑴𝑩𝑬𝒁𝑰 𝑲𝑨𝑻𝑰𝑲𝑨 𝑲𝑰𝑾𝑨𝑵𝑫𝑨 𝑪𝑯𝑨 𝑴𝑼𝑴𝑰𝑨𝑺 𝑵𝑨 𝑮𝑨𝑽𝑨𝑵𝑨 𝑩𝑨𝑹𝑨𝑺𝑨

Gavana Mchapakazi FCPA Fernandes Barasa amefanya ziara ya ghafla katika kiwanda cha kusaga sukari cha Mumias kushuhudia oparesheni zake.

Akizungumza na wanahabari katika kiwanda hicho, Gavana Barasa amewahimiza wakulima kuongeza upanzi wa miwa, akiahidi kuwa serikali yake itawasaidia kwa kuwapatia pembejeo kupitia kwa ushirikiano na kampuni hiyo.

Gavana Barasa pia amefichua kwamba kupitia ushirikiano wake na serikali kuu, madeni yote yanayoikabili kampuni hiyo, yapatayo shilingi bilioni 33, yatafutiliwa mbali hivi karibuni, kwani mswada huo upo bungeni tayari.

Meneja wa Oparesheni wa kampuni hiyo, Bw. Stephen Kirumba, alisema wameajiri maafisa wa kutoa mafunzo kwa wakulima ambao pia watasaidia katika kueneza ujumbe wa kukuza miwa eneo Zima la Kakamega na kwingineko.

Barasa alikuwa ameandamana na Mbunge wa Mumias Magharibi, Wawakilishi wa Wadi wakiongozwa na mwenyeji Mhe. Yassin Muchelule, Maafisa wa Kaunti wakiongozwa na Mkuu wa Wafanyikazi, Bw. Kassim Were, na wengine.