NewsTrending

𝑼𝑺𝑯𝑰𝑹𝑰𝑲𝑰𝑨𝑵𝑶 𝑾𝑨𝑵𝑮𝑼 𝑵𝑨 𝑹𝑨𝑰𝑺 𝑹𝑼𝑻𝑶 𝑼𝑻𝑨𝑲𝑨𝑴𝑰𝑳𝑰𝑺𝑯𝑨 𝑴𝑰𝑹𝑨𝑫𝑰 𝒀𝑨 𝑶𝑷𝑨𝑹𝑨𝑵𝒀𝑨, 𝑩𝑨𝑹𝑨𝑺𝑨 𝑨𝑬𝑳𝑬𝒁𝑨

Gavana Mchapakazi FCPA Fernandes Barasa katika ziara yake ya maendeleo kaunti ndogo ya Mumias Magharibi kwenye uwanja wa Matawa, Wadi ya Mumias ya Kati, amepigia debe ajenda zake sita kwa wakaazi wa Kakamega, akisema kupitia mpango huo wa kina, ameweza kufanikisha mengi na anatarajia kutimiza maendeleo zaidi katika kipindi chake cha uongozi cha miaka kumi.

Gavana huyo ameainisha kwamba ameupa kipaumbele mpango wa kukamilisha miradi yote iliyoanzishwa na mtangulizi wake, Mhe. Wycliffe Oparanya, kupitia ushirikiano wake na Rais William Ruto.

Miradi iliyoanzishwa na Gavana Oparanya, ambayo ushirikiano huo unalenga kukamilisha ni pamoja na Uwanja wa Kimataifa wa Bukhungu, Hospitali ya Ngazi ya Sita ya Kakamega, na miradi mingine inayogharimu mabilioni ya pesa.

Waliohudhuria ni pamoja na mbunge wa eneo hilo Mhe. Johnson Naicca, Wawakilishi wa Wadi wakiongozwa na Mhe. Ali Okomba (mwenyeji), Mbunge mtangulizi wa Mumias ya kale Mhe. Wycliffe Osundwa, maafisa wa serikali kuu na kaunti pamoja na wananchi.