NewsTrending

𝑼𝒁𝑰𝑡𝑫𝑼𝒁𝑰 𝑾𝑨 𝑩𝑨𝑹𝑨𝑩𝑨𝑹𝑨 𝑲𝑨𝑻𝑰𝑲𝑨 𝑾𝑨𝑫𝑰 𝒀𝑨 𝑰𝑫𝑨𝑲𝑯𝑢 𝑴𝑨𝑺𝑯𝑨𝑹𝑰𝑲𝑰

Ilikuwa zamu ya wananchi wa Kaunti Ndogo ya Ikolomani kunufaika na mipango kabambe ya Gavana Mchapakazi FCPA Fernandes Barasa alipozindua barabara ya Ivonda – Shule ya Msingi ya Ishianji β€” Kanisa la PCEA la Ishianji – Barabara ya Makutano ya Itsololi.

Mpango wa kuzindua barabara zenye urefu wa kilomita kumi katika kila wadi ni mojawapo ya mipangilio iliyopewa kipaumbele na Gavana huyo wa Jimbo la Kakamega.

Uzinduzi huo wa barabara unalenga kuchangia uboreshaji wa kiwango cha maisha ya wananchi wa Kakamega kwa kuchochea biashara na mawasiliano.

Gavana Barasa alikuwa ameandamana na Wawakilishi wa Wadi, wakiongozwa na Mhe. Silas Shiyenji (Mwenyeji), Maafisa wa Kaunti, Watawala wa Serikali Kuu na Kaunti, na wananchi wa eneo hilo.