𝑲𝑰𝑱𝑰𝑱𝑰 𝑪𝑯𝑨 𝑬𝑳𝑾𝑨𝑲𝑨𝑵𝑨 𝑪𝑯𝑨𝑵𝑮’𝑨𝑨 𝑲𝑾𝑨 𝑼𝑴𝑬𝑴𝑬 𝑾𝑨 𝑩𝑨𝑹𝑨𝑺𝑨.
𝐈𝐣𝐮𝐦𝐚𝐚, 𝐉𝐚𝐧𝐮𝐚𝐫𝐢 𝟓, 𝟐𝟎𝟐𝟒.
Leo, wanakijiji wa Elwakana, Bumwende, Kaunti ndogo ya Mumias Mashariki, wamejawa na furaha baada ya Gavana Mchapakazi FCPA Fernandes Barasa kutimiza ahadi yake ya kampeni kwa kuwaletea transfoma yenye uwezo wa kusambaza umeme pia katika maeneo jirani.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuzinduwa rasmi umeme huo kwa wananchi, Gavana Barasa alifichua kwamba aliamua kuwasha mwangaza huo mwenyewe kama ishara ya shukrani kwa wananchi na wanakijiji hao, ambao wamekosa umeme kwa miaka mingi.
Mwaka jana, Gavana Barasa, akiwa katika jitihada za kuzalisha nishati Kakamega nzima, alikutana na wasimamizi wa kampuni ya uzalishaji umeme kupitia teknolojia ya nishati mbadala, inayojulikana kama “Hydrobox.” Kampuni hii itazalisha umeme katika Jimbo la Kakamega, hususan maeneo yenye mito.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Wawakilishi wa Wadi wakiongozwa na Mhe. Timothy Anzetse (mwenyeji), Maafisa wa Kaunti wakiwemo Mawaziri, Maafisa Wakuu, Watawala wa serikali kuu na kaunti, pamoja na wananchi.