𝑵𝑰𝑻𝑨𝑺𝑯𝑰𝑹𝑰𝑲𝑰𝑨𝑵𝑨 𝑵𝑨 𝑩𝑨𝑹𝑨𝑺𝑨 𝑲𝑼𝑴𝑨𝑳𝑰𝒁𝑨 𝑼𝑱𝑬𝑵𝒁𝑰 𝑾𝑨 𝑩𝑼𝑲𝑯𝑼𝑵𝑮𝑼, 𝑾𝑨𝒁𝑰𝑹𝑰 𝑵𝑨𝑴𝑾𝑨𝑴𝑩𝑨 𝑨𝑻𝑶𝑨 𝑨𝑯𝑨𝑫𝑰
𝐉𝐮𝐦𝐚𝐭𝐚𝐧𝐨, 𝐉𝐚𝐧𝐮𝐚𝐫𝐢 𝟑, 𝟐𝟎𝟐𝟒.
Kama njia ya kukuza michezo na kuendeleza vipaji katika Jimbo la Kakamega, Gavana Mchapakazi FCPA Fernandes Barasa amemkaribisha Waziri wa Michezo, Mhe. Ababu Namwamba, katika uwanja wa Lugala, Wadi ya Isukha ya Kati, katika fainali ya Kombe la Mjumbe wa eneo la Shinyalu, Mhe. Fred Ikana.
Katika hotuba yake, Gavana Barasa amemshukuru Waziri Namwamba kwa kutoa hakikisho kwamba Serikali Kuu imejitolea kushirikiana na Serikali ya Kakamega kumaliza ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Bukhungu, akifichua kwamba serikali yake imewekeza shilingi milioni 530 mwaka huu wa kifedha 2023/2024 kwa ukamilishaji wa uwanja huo.
Kadhalika, Gavana huyo ambaye anaongoza Magavana wenziwe katika utendakazi nchini kulingana na utafiti wa shirika la Politrack, amepongeza washindi wa leo, Leone FC, kwa kuwapiku Shisokoro FC bao moja kwa sifuri na kuutwaa ubingwa wa soka ya wavulana, huku Tarino wakiridhika na nafasi ya tatu. Shinyalu Queens wameshinda soka ya akina dada kwa kuwachabanga Museno Queens huku Juventus wakichukua nafasi ya tatu.
Wageni waliohudhuria ni pamoja na: Wabunge Bernard Shinali (Ikolomani), Innocent Mugabe (Likuyani) na Malulu Injendi (Malava), Wawakilishi wa Wadi wakiongozwa na Mhe. Dan Mukofu wa Isukha ya kati, Maafisa wa Kaunti wakiongozwa na Waziri Rachel Atamba (Biashara, Uendelezaji wa Viwanda, na Utalii), wapenzi wa spoti, na nwengineo.