NewsTrending

𝑴𝑨𝑺𝑶𝑴𝑶 𝒀𝑨 𝑪𝑯𝑬𝑲𝑬𝑪𝑯𝑬𝑨 𝑲𝑼𝑰𝑴𝑨𝑹𝑰𝑲𝑨 𝑮𝑨𝑽𝑨𝑵𝑨 𝑩𝑨𝑹𝑨𝑺𝑨 𝑨𝑲𝑰𝑻𝑨𝑵𝑮𝑨𝒁𝑨 𝑲𝑼𝑹𝑨𝑺𝑰𝑴𝑰𝑺𝑯𝑨 𝑴𝑨𝑻𝑼𝑴𝑰𝒁𝑰 𝒀𝑨 𝑴𝑨𝑫𝑨𝑹𝑨𝑺𝑨.

𝐉𝐮𝐦𝐚𝐦𝐨𝐬𝐢, 𝐉𝐚𝐧𝐮𝐚𝐫𝐢 𝟔, 𝟐𝟎𝟐𝟒.
Gavana Mchapakazi FCPA Fernandes Barasa ametangaza kwamba ataanza kurasimisha matumizi ya madarasa ya Elimu ya Chekechea (ECDE) ambayo ujenzi wao umekamilika hivi karibuni, ili kuwapa wanafunzi nafasi ya kupata elimu katika mazingira bora. Hii inaambatana na nguzo yake ya nne ya kuboresha elimu.

Barasa aliyasema hayo wakati wa mazishi ya Mama Wilbroda Ometi, katika Shule ya Msingi ya Bukosi, wadi ya Mayoni, Kaunti ndogo ya Matungu, huku akimwomboleza marehemu kama mcha Mungu ambaye ameacha mfano mwema kwa vizazi vya sasa.

Kaunti ya Kakamega imemaliza ujenzi wa madarasa 46 chini ya uongozi wa Gavana Barasa na mengine yakiwa katika vitengo mbalimbali vya ujenzi.

Serikali ya Gavana Barasa pia imewekeza shilingi milioni mia mbili sabini Na tatu, elfu mia tano ili kuboresha masomo ya elimu ya chekechea mwaka huu wa kifedha 2023/2024.

Kwa mara nyingine, Gavana Barasa aliwaomba wanafunzi wa sekondari, vyuo vya ufundi vya kaunti pamoja na vyuo vya ualimu wa elimu ya chekechea, kuchukua fursa hii na kufanya maombi ya ufadhili wa masomo, kabla ya muda wa kufanya hivyo kukamilika ijumaa ijayo.

Walioambatana na Gavana ni pamoja na mkuu wa bodi ya Shirika la Mamlaka ya Mabonde ya Maji nchini Kenya, Bw. Rashid Echesa, Maafisa wa Kaunti wakiwemo Mawaziri, Maafisa Wakuu, na watawala wa serikali kuu na kaunti.