πΌππ°π΅π«πΌππ° πΎπ¨ π΄π¨π«π¨πΉπ¨πΊπ¨ ππ¨ πͺπ―π¬π²π¬πͺπ―π¬π¨; π°π«π¨π²π―πΆ π²πΌπΊπ°π΅π°.
Kwa kuzingatia ajenda yake ya nne ya kuboresha elimu katika jimbo la Kakamega kwa kuchochea mazingira bora, Gavana Mchapakazi FCPA Fernandes Barasa amejiunga na washikadau wa Shule ya Msingi ya Ikhulili, wakiwapo: Wanafunzi, walimu, na wazazi, ambapo amezindua madarasa ya chekechea katika shule hiyo.
Akizungumza katika shule hiyo, Gavana Barasa amepigia upato mpango wake wa ugavi wa basari, unaogharimu shilingi milioni 240, akimwelekeza Waziri wa Elimu wa Kaunti, Dkt. Boniface Okoth, kuwapa kipaumbele wanafunzi wasiojiweza kwa kuhakikisha wanafaidika vizuri na fursa za elimu.
Gavana Barasa alipokelewa na Wawakilishi wa Wadi wakiongozwa na Mhe. Stephen Mukhala, Maafisa wa Kaunti, Walimu, pamoja na wazazi.