Sunday, July 13, 2025
Latest:
NewsTrending

𝑼𝒁𝑰𝑵𝑫𝑼𝒁𝑰 𝑾𝑨 𝑴𝑨𝑫𝑨𝑹𝑨𝑺𝑨 𝒀𝑨 𝑪𝑯𝑬𝑲𝑬𝑪𝑯𝑬𝑨; 𝑰𝑫𝑨𝑲𝑯𝑶 𝑲𝑨𝑺𝑲𝑨𝒁𝑰𝑵𝑰

Katika ziara yake ya maendeleo Kaunti ndogo ya Ikolomani, Gavana Mchapakazi FCPA Fernandes Barasa amezindua madarasa ya chekechea katika Shule ya Shichinji.

Akiwa ameandamana na Maafisa wa serikali yake, Barasa alipokelewa na Wawakilishi Wadi mbalimbali, akiwapo Mhe. Gladys Omukongolo (Mwenyeji), ambapo alisema ana nia ya kuinua kiwango cha elimu eneo hilo, na jimbo zima la Kakamega, ikiwamo kuinua hadhi ya Chuo cha Elimu cha Eregi hadi kuwa chuo kikuu kwa ushirikiano na serikali kuu.